بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ
Kwa jina la Allah Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu

Assalaam Aleyikum,

Ndugu msomaji wa website hii sinabudi kumshukuru Allah (s.w) kwa kunipa taufiq ya kutayarisha na kukuandalia ukurasa huu wa www.somaquran.com

Lengo na makusudio yetu kwako wewe msomaji wetu ni kuurejesha moyo wako na fikra zako katika kumjua Yule aliyeumba mbingu na ardhi, na lengo la Yeye kukuumba wewe mwanadamu!

Ndugu msomaji utayajua makusudio hayo kwa kuisoma Quran tukufu na tafsiri yake (maana yake) ili uweze kupata muongozo sahihi wa maisha yako pamoja na jamii yote kwa ujumla.

Ndugu msomaji tafsiri hii ya quran tukufu ni tarjama ya Kiswahili ambayo tumeinakili kutoka katika tafsiri ya Sheikh Hassan Ally Mwalupa, hivyo ikiwa utabaini ikhtilafu yoyote katika tafsiri hii basi usisite kutoa maoni yako kwetu, nasi Inshaallah tutayafanyia kazi Bi Idhnillahi Taalah! Kwani hakuna Mkamilifu sipokuwa Yeye Peke Yake Allah (s.w.t).

Namuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu aijalie kazi hii iwe ni kwa ajili ya kutaka radhi Zake, na Atujalie sote tuwe ni wenye kupata manufaa makubwa kwa kuisoma hii Quran na kupata mazingatio Yake hapa duniani na akhera.

Wabillah Taufiq.

Soma Quran Team.
Barua Pepe: info@somaquran.com.