Sura 55 - Ar-Rahmaan

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ
Kwa Jina La Mwenyezi Mungu, Mwingi Wa Rehema, Mwenye Kurehemu.

55:1
الرَّحْمَٰنُ
*Arrah´man, Mwingi wa Rehema
*The All-beneficent
55:2
عَلَّمَ الْقُرْآنَ
*Amefundisha Qur´ani.
*has taught the Quran.
55:3
خَلَقَ الْإِنْسَانَ
*Amemuumba mwanaadamu,
*He created man,
55:4
عَلَّمَهُ الْبَيَانَ
*Akamfundisha kubaini.
*[and] taught him articulate speech.
55:5
الشَّمْسُ وَالْقَمَرُ بِحُسْبَانٍ
*Jua na mwezi huenda kwa hisabu.
*The sun and the moon are [disposed] calculatedly,
55:6
وَالنَّجْمُ وَالشَّجَرُ يَسْجُدَانِ
*Na mimea yenye kutambaa, na miti, inanyenyekea.
*and the herb and the tree prostrate [to Allah].
55:7
وَالسَّمَاءَ رَفَعَهَا وَوَضَعَ الْمِيزَانَ
*Na mbingu ameziinua, na ameweka mizani,
*He raised the heaven high and set up the balance,
55:8
أَلَّا تَطْغَوْا فِي الْمِيزَانِ
*Ili msidhulumu katika mizani.
*declaring, ‘Do not infringe the balance!
55:9
وَأَقِيمُوا الْوَزْنَ بِالْقِسْطِ وَلَا تُخْسِرُوا الْمِيزَانَ
*Na wekeni mizani kwa haki, wala msipunje katika mizani.
*Maintain the weights with justice, and do not shorten the balance!’
55:10
وَالْأَرْضَ وَضَعَهَا لِلْأَنَامِ
*Na ardhi ameiweka kwa ajili ya viumbe.
*And the earth—He laid it out for mankind.
55:11
فِيهَا فَاكِهَةٌ وَالنَّخْلُ ذَاتُ الْأَكْمَامِ
*Humo yamo matunda na mitende yenye mafumba.
*In it are fruits and date-palms with sheaths,
55:12
وَالْحَبُّ ذُو الْعَصْفِ وَالرَّيْحَانُ
*Na nafaka zenye makapi, na rehani.
*grain with husk, and fragrant herbs.
55:13
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
*Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha
*So which of your Lord’s bounties will you both deny?
55:14
خَلَقَ الْإِنْسَانَ مِنْ صَلْصَالٍ كَالْفَخَّارِ
*Amemuumba mtu kwa udongo wa kinamo..
*He created man out of dry clay, like the potter’s,
55:15
وَخَلَقَ الْجَانَّ مِنْ مَارِجٍ مِنْ نَارٍ
*Na akawaumba majini kwa ulimi wa moto.
*and created the jinn out of a flame of a fire.
55:16
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
*Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha
*So which of your Lord’s bounties will you both deny?
55:17
رَبُّ الْمَشْرِقَيْنِ وَرَبُّ الْمَغْرِبَيْنِ
*Mola Mlezi wa mashariki mbili na wa magharibi mbili.
*Lord of the two easts, and Lord of the two wests!
55:18
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
*Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
*So which of your Lord’s bounties will you both deny?
55:19
مَرَجَ الْبَحْرَيْنِ يَلْتَقِيَانِ
*Anaziendesha bahari mbili zikutane;
*He merged the two seas, meeting each other.
55:20
بَيْنَهُمَا بَرْزَخٌ لَا يَبْغِيَانِ
*Baina yao kipo kizuizi, zisiingiliane.
*There is a barrier between them, which they do not overstep.
55:21
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
*Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
*So which of your Lord’s bounties will you both deny?
55:22
يَخْرُجُ مِنْهُمَا اللُّؤْلُؤُ وَالْمَرْجَانُ
*Katika hizo bahari mbili zinatoka lulu na marijani.
*From them emerge the pearl and the coral.
55:23
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
*Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
*So which of your Lord’s bounties will you both deny?
55:24
وَلَهُ الْجَوَارِ الْمُنْشَآتُ فِي الْبَحْرِ كَالْأَعْلَامِ
*Na ni vyake Yeye hivi viendavyo baharini vilivyo undwa kama vilima.
*His are the sailing ships on the sea [appearing] like landmarks.
55:25
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
*Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
*So which of your Lord’s bounties will you both deny?
55:26
كُلُّ مَنْ عَلَيْهَا فَانٍ
*Kila kilioko juu yake kitatoweka.
*Everyone on it is ephemeral,
55:27
وَيَبْقَىٰ وَجْهُ رَبِّكَ ذُو الْجَلَالِ وَالْإِكْرَامِ
*Na atabakia Mwenyewe Mola wako Mlezi Mwenye utukufu na ukarimu.
*yet lasting is the majestic and munificent Face of your Lord.
55:28
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
*Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
*So which of your Lord’s bounties will you both deny?
55:29
يَسْأَلُهُ مَنْ فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۚ كُلَّ يَوْمٍ هُوَ فِي شَأْنٍ
*Vinamwomba Yeye vilivyomo katika mbingu na ardhi. Kila siku Yeye yumo katika mambo.
*Everyone in the heavens and the earth asks Him. Every day He is engaged in some work.
55:30
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
*Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
*So which of your Lord’s bounties will you both deny?
55:31
سَنَفْرُغُ لَكُمْ أَيُّهَ الثَّقَلَانِ
*Tutakuhisabuni enyi makundi mawili.
*Soon We shall make Ourselves unoccupied for you, O you notable two!
55:32
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
*Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
*So which of your Lord’s bounties will you both deny?
55:33
يَا مَعْشَرَ الْجِنِّ وَالْإِنْسِ إِنِ اسْتَطَعْتُمْ أَنْ تَنْفُذُوا مِنْ أَقْطَارِ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ فَانْفُذُوا ۚ لَا تَنْفُذُونَ إِلَّا بِسُلْطَانٍ
*Enyi makundi ya majini na watu! Mkiweza kupenya kwenye mbingu na ardhi, basi penyeni! Hamtapenya ila kwa kupewa madaraka.
*O company of jinn and humans! If you can pass through the confines of the heavens and the earth, then do pass through. But you will not pass through except by an authority [from Allah].
55:34
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
*Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
*So which of your Lord’s bounties will you both deny?
55:35
يُرْسَلُ عَلَيْكُمَا شُوَاظٌ مِنْ نَارٍ وَنُحَاسٌ فَلَا تَنْتَصِرَانِ
*Mtapelekewa muwako wa moto na shaba; wala hamtashinda.
*There will be unleashed upon you a flash of fire and a smoke; then you will not be able to help one another.
55:36
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
*Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
*So which of your Lord’s bounties will you both deny?
55:37
فَإِذَا انْشَقَّتِ السَّمَاءُ فَكَانَتْ وَرْدَةً كَالدِّهَانِ
*Itakapo pasuka mbingu ikawa nyekundu kama mafuta.
*When the sky is split open, and turns crimson like tanned leather.
55:38
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
*Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
*So which of your Lord’s bounties will you both deny?
55:39
فَيَوْمَئِذٍ لَا يُسْأَلُ عَنْ ذَنْبِهِ إِنْسٌ وَلَا جَانٌّ
*Siku hiyo hataulizwa dhambi zake mtu wala jini.
*On that day neither humans will be questioned about their sins nor jinn.
55:40
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
*Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
*So which of your Lord’s bounties will you both deny?
55:41
يُعْرَفُ الْمُجْرِمُونَ بِسِيمَاهُمْ فَيُؤْخَذُ بِالنَّوَاصِي وَالْأَقْدَامِ
*Watajuulikana wakosefu kwa alama zao, basi watashikwa kwa nywele zao za utosini na kwa miguu.
*The guilty will be recognized by their mark; so they will be seized by their forelocks and feet.
55:42
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
*Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
*So which of your Lord’s bounties will you both deny?
55:43
هَٰذِهِ جَهَنَّمُ الَّتِي يُكَذِّبُ بِهَا الْمُجْرِمُونَ
*Hii ndiyo Jahannamu ambayo wakosefu wakiikanusha.
*‘This is the hell which the guilty would deny!’
55:44
يَطُوفُونَ بَيْنَهَا وَبَيْنَ حَمِيمٍ آنٍ
*Watakuwa wakizunguka baina ya hiyo na maji ya moto yanayo chemka.
*They shall circuit between it and boiling hot water.
55:45
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
*Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
*So which of your Lord’s bounties will you both deny?
55:46
وَلِمَنْ خَافَ مَقَامَ رَبِّهِ جَنَّتَانِ
*Na mwenye kuogopa kusimamishwa mbele ya Mola wake Mlezi atapata Bustani mbili.
*For him who stands in awe of his Lord will be two gardens.
55:47
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
*Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
*So which of your Lord’s bounties will you both deny?
55:48
ذَوَاتَا أَفْنَانٍ
*Bustani zenye matawi yaliyo tanda.
*Both abounding in branches.
55:49
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
*Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
*So which of your Lord’s bounties will you both deny?
55:50
فِيهِمَا عَيْنَانِ تَجْرِيَانِ
*Ndani yake zimo chemchem mbili zinazo pita.
*In both of them will be two flowing springs.
55:51
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
*Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
*So which of your Lord’s bounties will you both deny?
55:52
فِيهِمَا مِنْ كُلِّ فَاكِهَةٍ زَوْجَانِ
*Humo katika kila matunda zimo namna mbili.
*In both of them will be two kinds of every fruit.
55:53
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
*Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
*So which of your Lord’s bounties will you both deny?
55:54
مُتَّكِئِينَ عَلَىٰ فُرُشٍ بَطَائِنُهَا مِنْ إِسْتَبْرَقٍ ۚ وَجَنَى الْجَنَّتَيْنِ دَانٍ
*Wawe wameegemea matandiko yenye bit´ana ya hariri nzito; na matunda ya Bustani hizo yapo karibu.
*[They will be] reclining on beds lined with green silk. And the fruit of the two gardens will be near at hand.
55:55
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
*Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
*So which of your Lord’s bounties will you both deny?
55:56
فِيهِنَّ قَاصِرَاتُ الطَّرْفِ لَمْ يَطْمِثْهُنَّ إِنْسٌ قَبْلَهُمْ وَلَا جَانٌّ
*Humo watakuwamo wanawake watulizao macho yao; hajawagusa mtu kabla yao wala jini.
*In them are maidens of restrained glances, whom no human has touched before, nor jinn.
55:57
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
*Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
*So which of your Lord’s bounties will you both deny?
55:58
كَأَنَّهُنَّ الْيَاقُوتُ وَالْمَرْجَانُ
*Kama kwamba wao ni yakuti na marijani.
*As though they were rubies and corals.
55:59
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
*Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha.
*So which of your Lord’s bounties will you both deny?
55:60
هَلْ جَزَاءُ الْإِحْسَانِ إِلَّا الْإِحْسَانُ
*Ati yaweza kuwa malipo ya ihsani ila ihsani?
*Is the requital of goodness anything but goodness?
55:61
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
*Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
*So which of your Lord’s bounties will you both deny?
55:62
وَمِنْ دُونِهِمَا جَنَّتَانِ
*Na zaidi ya hizo zipo Bustani nyengine mbili.
*Beside these two, there will be two [other] gardens.
55:63
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
*Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
*So which of your Lord’s bounties will you both deny?
55:64
مُدْهَامَّتَانِ
*Za kijani kibivu.
*Dark green.
55:65
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
*Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
*So which of your Lord’s bounties will you both deny?
55:66
فِيهِمَا عَيْنَانِ نَضَّاخَتَانِ
*Na chemchem mbili zinazo furika.
*In both of them will be two gushing springs.
55:67
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
*Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
*So which of your Lord’s bounties will you both deny?
55:68
فِيهِمَا فَاكِهَةٌ وَنَخْلٌ وَرُمَّانٌ
*Imo humo miti ya matunda, na mitende na mikomamanga.
*In both of them will be fruits, date-palms and pomegranates.
55:69
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
*Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
*So which of your Lord’s bounties will you both deny?
55:70
فِيهِنَّ خَيْرَاتٌ حِسَانٌ
*Humo wamo wanawake wema wazuri.
*In them are maidens good and lovely.
55:71
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
*Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
*So which of your Lord’s bounties will you both deny?
55:72
حُورٌ مَقْصُورَاتٌ فِي الْخِيَامِ
*Wanawake wazuri wanao tawishwa katika makhema.
*Houris secluded in pavilions.
55:73
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
*Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
*So which of your Lord’s bounties will you both deny?
55:74
لَمْ يَطْمِثْهُنَّ إِنْسٌ قَبْلَهُمْ وَلَا جَانٌّ
*Hajawagusa mtu wala jini kabla yao.
*Whom no human has touched before, nor jinn.
55:75
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
*Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
*So which of your Lord’s bounties will you both deny?
55:76
مُتَّكِئِينَ عَلَىٰ رَفْرَفٍ خُضْرٍ وَعَبْقَرِيٍّ حِسَانٍ
*Wameegemea juu ya matakia ya kijani na mazulia mazuri.
*Reclining on green cushions and lovely carpets.
55:77
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
*Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
*So which of your Lord’s bounties will you both deny?
55:78
تَبَارَكَ اسْمُ رَبِّكَ ذِي الْجَلَالِ وَالْإِكْرَامِ
*Limetukuka jina la Mola wako Mlezi Mwenye utukufu na ukarimu.
*Blessed is the Name of your Lord, the Majestic and the Munificent!