Sura 100 - Al-Aadiyaat

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ
Kwa Jina La Mwenyezi Mungu, Mwingi Wa Rehema, Mwenye Kurehemu.

100:1
وَالْعَادِيَاتِ ضَبْحًا
*Naapa kwa farasi wendao mbio wakipumua,
*By the snorting chargers,
100:2
فَالْمُورِيَاتِ قَدْحًا
*Na wakitoa moto kwa kupiga kwato zao chini,
*by the strikers of sparks [with their hoofs],
100:3
فَالْمُغِيرَاتِ صُبْحًا
*Wakishambulia wakati wa asubuhi,
*by the raiders at dawn,
100:4
فَأَثَرْنَ بِهِ نَقْعًا
*Huku wakitimua vumbi,
*raising therein a trail of dust,
100:5
فَوَسَطْنَ بِهِ جَمْعًا
*Na wakijitoma kati ya kundi,
*and cleaving therein a host!
100:6
إِنَّ الْإِنْسَانَ لِرَبِّهِ لَكَنُودٌ
*Hakika mwanaadamu ni mtovu wa fadhila kwa Mola wake Mlezi!
*Indeed man is ungrateful to his Lord,
100:7
وَإِنَّهُ عَلَىٰ ذَٰلِكَ لَشَهِيدٌ
*Na hakika yeye mwenyewe bila ya shaka ni shahidi wa hayo!
*and indeed he is [himself] witness to that!
100:8
وَإِنَّهُ لِحُبِّ الْخَيْرِ لَشَدِيدٌ
*Naye hakika bila ya shaka ana nguvu za kupenda mali!
*And indeed he is an avid lover of wealth.
100:9
أَفَلَا يَعْلَمُ إِذَا بُعْثِرَ مَا فِي الْقُبُورِ
*Kwani hajui watakapo fufuliwa waliomo makaburini?
*Does he not know, when what is [buried] in the graves is turned over,
100:10
وَحُصِّلَ مَا فِي الصُّدُورِ
*Na yakakusanywa yaliomo vifuani?
*and what is [concealed] in the breasts is divulged,
100:11
إِنَّ رَبَّهُمْ بِهِمْ يَوْمَئِذٍ لَخَبِيرٌ
*Kuwa hakika Mola wao Mlezi siku hiyo bila ya shaka atakuwa na khabari zao wote!
*on that day their Lord will be well informed about them [and their deeds]?