Sura 79 - An-Naazi'aat

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ
Kwa Jina La Mwenyezi Mungu, Mwingi Wa Rehema, Mwenye Kurehemu.

79:1
وَالنَّازِعَاتِ غَرْقًا
*Naapa kwa wanao komoa kwa nguvu,
*By those [angels] who wrest [the soul] violently,
79:2
وَالنَّاشِطَاتِ نَشْطًا
*Na kwa wanao toa kwa upole,
*by those who draw [it] out gently,
79:3
وَالسَّابِحَاتِ سَبْحًا
*Na wanao ogelea,
*by those who swim smoothly,
79:4
فَالسَّابِقَاتِ سَبْقًا
*Wakishindana mbio,
*by those who, racing, take the lead,
79:5
فَالْمُدَبِّرَاتِ أَمْرًا
*Wakidabiri mambo.
*by those who direct the affairs [of creatures]:
79:6
يَوْمَ تَرْجُفُ الرَّاجِفَةُ
*Siku kitapo tetemeka cha kutetemeka,
*the day when the Quaker quakes
79:7
تَتْبَعُهَا الرَّادِفَةُ
*Kifuate cha kufuatia.
*and is followed by the Successor,
79:8
قُلُوبٌ يَوْمَئِذٍ وَاجِفَةٌ
*Siku hiyo nyoyo zitapiga piga,
*hearts will be trembling on that day,
79:9
أَبْصَارُهَا خَاشِعَةٌ
*Macho yatainama chini.
*bearing a humbled look.
79:10
يَقُولُونَ أَإِنَّا لَمَرْدُودُونَ فِي الْحَافِرَةِ
*Sasa wanasema: Ati kweli tutarudishwa kwenye hali ya kwanza?
*They will say, ‘Are we being returned to our earlier state?
79:11
أَإِذَا كُنَّا عِظَامًا نَخِرَةً
*Hata tukiwa mifupa iliyo bunguliwa?
*What, even after we have been decayed bones?!’
79:12
قَالُوا تِلْكَ إِذًا كَرَّةٌ خَاسِرَةٌ
*Wanasema: Basi marejeo hayo ni yenye khasara!
*They will say, ‘This is, then, a ruinous return!’
79:13
فَإِنَّمَا هِيَ زَجْرَةٌ وَاحِدَةٌ
*Kwa hakika hayo ni ukelele mmoja tu,
*Yet it will be only a single shout,
79:14
فَإِذَا هُمْ بِالسَّاهِرَةِ
*Mara watakuwa kwenye uwanda wa mkutano!
*and behold, they will be awake.
79:15
هَلْ أَتَاكَ حَدِيثُ مُوسَىٰ
*Je! Imekufikia hadithi ya Musa?
*Did you receive the story of Moses,
79:16
إِذْ نَادَاهُ رَبُّهُ بِالْوَادِ الْمُقَدَّسِ طُوًى
*Mola wake Mlezi alipo mwita katika bonde takatifu la T´uwaa, akamwambia:
*when his Lord called out to him in the holy valley of Tuwa?
79:17
اذْهَبْ إِلَىٰ فِرْعَوْنَ إِنَّهُ طَغَىٰ
*Nenda kwa Firauni. Hakika yeye amezidi jeuri.
*[And said,] ‘Go to Pharaoh, for indeed he has rebelled,
79:18
فَقُلْ هَلْ لَكَ إِلَىٰ أَنْ تَزَكَّىٰ
*Umwambie: Je! Unapenda kujitakasa?
*and say, ‘‘Would you purify yourself?
79:19
وَأَهْدِيَكَ إِلَىٰ رَبِّكَ فَتَخْشَىٰ
*Nami nitakuongoa ufike kwa Mola wako Mlezi, upate kumcha.
*I will guide you to your Lord, that you may fear [Him]?’’ ’
79:20
فَأَرَاهُ الْآيَةَ الْكُبْرَىٰ
*Basi alimwonyesha Ishara kubwa.
*Then he showed him the greatest sign.
79:21
فَكَذَّبَ وَعَصَىٰ
*Lakini aliikadhibisha na akaasi.
*But he denied, and disobeyed.
79:22
ثُمَّ أَدْبَرَ يَسْعَىٰ
*Kisha alirudi nyuma, akaingia kufanya juhudi.
*Then he turned back, walking swiftly,
79:23
فَحَشَرَ فَنَادَىٰ
*Akakusanya watu akanadi.
*and gathered [the people] and proclaimed,
79:24
فَقَالَ أَنَا رَبُّكُمُ الْأَعْلَىٰ
*Akasema: Mimi ndiye Mola wenu Mlezi mkuu kabisa.
*saying, ‘I am your exalted lord!’
79:25
فَأَخَذَهُ اللَّهُ نَكَالَ الْآخِرَةِ وَالْأُولَىٰ
*Basi hapo Mwenyezi Mungu akamshika kumuadhibu kwa la mwisho na la mwanzo.
*So Allah seized him with the punishment of this life and the Hereafter.
79:26
إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَعِبْرَةً لِمَنْ يَخْشَىٰ
*Kwa hakika katika haya yapo mazingatio kwa wanao ogopa.
*There is indeed a moral in that for someone who fears!
79:27
أَأَنْتُمْ أَشَدُّ خَلْقًا أَمِ السَّمَاءُ ۚ بَنَاهَا
*Je! Ni vigumu zaidi kukuumbeni nyinyi au mbingu? Yeye ndiye aliye ijenga!
*Is your creation more prodigious or that of the heaven He has built?
79:28
رَفَعَ سَمْكَهَا فَسَوَّاهَا
*Akainua kimo chake, na akaitengeneza vizuri.
*He raised its vault and fashioned it,
79:29
وَأَغْطَشَ لَيْلَهَا وَأَخْرَجَ ضُحَاهَا
*Na akautia giza usiku wake, na akautokeza mchana wake.
*and darkened its night, and brought forth its forenoon.
79:30
وَالْأَرْضَ بَعْدَ ذَٰلِكَ دَحَاهَا
*Na juu ya hivyo ameitandaza ardhi.
*Thereafter He spread out the earth,
79:31
أَخْرَجَ مِنْهَا مَاءَهَا وَمَرْعَاهَا
*Akatoa ndani yake maji yake na malisho yake,
*brought forth from it its water and pastures,
79:32
وَالْجِبَالَ أَرْسَاهَا
*Na milima akaisimamisha,
*setting firm the mountains,
79:33
مَتَاعًا لَكُمْ وَلِأَنْعَامِكُمْ
*Kwa nafuu yenu na mifugo yenu.
*as a [place of] sustenance for you and your livestock.
79:34
فَإِذَا جَاءَتِ الطَّامَّةُ الْكُبْرَىٰ
*Basi itakapo fika hiyo balaa kubwa,
*When the Greatest Catastrophe befalls
79:35
يَوْمَ يَتَذَكَّرُ الْإِنْسَانُ مَا سَعَىٰ
*Siku ambayo mtu atakumbuka aliyo yafanya,
*—the day when man will remember his endeavours
79:36
وَبُرِّزَتِ الْجَحِيمُ لِمَنْ يَرَىٰ
*Na Jahannamu itadhihirishwa kwa mwenye kuona,
*and hell is brought into view for those who can see—
79:37
فَأَمَّا مَنْ طَغَىٰ
*Basi ama yule aliye zidi ujeuri,
*as for him who has been rebellious
79:38
وَآثَرَ الْحَيَاةَ الدُّنْيَا
*Na akakhiari maisha ya dunia,
*and preferred the life of this world,
79:39
فَإِنَّ الْجَحِيمَ هِيَ الْمَأْوَىٰ
*Kwa hakika Jahannamu ndiyo makaazi yake!
*his refuge will indeed be hell.
79:40
وَأَمَّا مَنْ خَافَ مَقَامَ رَبِّهِ وَنَهَى النَّفْسَ عَنِ الْهَوَىٰ
*Na ama yule anaye ogopa kusimamishwa mbele ya Mola wake Mlezi, na akajizuilia nafsi yake na matamanio,
*But as for him who is awed to stand before his Lord and restrains his soul from [following] desires,
79:41
فَإِنَّ الْجَنَّةَ هِيَ الْمَأْوَىٰ
*Basi huyo, Pepo itakuwa ndiyo makaazi yake!
*his refuge will indeed be paradise.
79:42
يَسْأَلُونَكَ عَنِ السَّاعَةِ أَيَّانَ مُرْسَاهَا
*Wanakuuliza Saa (ya Kiyama) itakuwa lini?
*They ask you concerning the Hour, “When will it set in,
79:43
فِيمَ أَنْتَ مِنْ ذِكْرَاهَا
*Una nini wewe hata uitaje?
*considering your frequent mention of it?”
79:44
إِلَىٰ رَبِّكَ مُنْتَهَاهَا
*Kwa Mola wako Mlezi ndio mwisho wake.
*Its outcome is with your Lord.
79:45
إِنَّمَا أَنْتَ مُنْذِرُ مَنْ يَخْشَاهَا
*Kwa hakika wewe ni mwonyaji tu kwa mwenye kuikhofu.
*You are only a warner for those who are afraid it.
79:46
كَأَنَّهُمْ يَوْمَ يَرَوْنَهَا لَمْ يَلْبَثُوا إِلَّا عَشِيَّةً أَوْ ضُحَاهَا
*Ni kama kwamba wao siku watapo iona (hiyo Saa) hawakukaa ila jioni moja tu, au mchana wake.
*The day they see it, it shall be as if they had not stayed [in the world] except for an evening or forenoon.